Wednesday, 2 March 2011

Kwanini Kikwete anapenda kuficha anaoandamanao nje?


Sijui ni mazoea au niseme haki. Rais wa nchi anapokuwa ziarani nje ya nchi, ni vizuri umma ukajulisha waliomo kwenye ujumbe wake.

Tulizoea kusoma majina ya waliondamana na rais nje ya nchi awamu zote zilizopita.
Tangu rais Jakaya Kikwete aingie madarakani na kuanza kuandamana na watu wanaotia shaka kwenye ziara zake, kumekuwa na ufichaji wa orodha ya watu wanaoandamana naye nje ya nchi. Je anaficha nini kama hakuna namna? Mchezo mzima ulianza baada ya kipindi fulani vyombo vya habari kustukia Kikwete kuandamana na wana familia yake kwenye mkutano wa umoja wa mataifa huko New York kwa gharama ya mlipa kodi maskini.

Walipakodi wanaomwezesha kufanya haya matanuzi wanapaswa kujua anaoandamana nao rais ili kama kuna wasiofaa aelezwe hivyo sivyo.

Wachambuzi chunguzeni tujue sababu ya Kikwete kuficha majina ya watu anaoandamana nao kwenye msafara nje aendapo kufanya u-Vasco da Gama.

2 comments:

Anonymous said...

Hiki kijamaa kinaweza kuwa kinaandamana na vimada wake.

Anonymous said...

unadhani atakwambia vimada anaoenda nae nje? thubutu! huyo ndo mkwere bana