Thursday, 10 March 2011

Kikwete na Mkapa watunukiwa shahada ya aina yakeKwa vile watawala wetu ni wapenzi wa shahada za dezo zitolewazo na vyuo vyenye kutia kila aina ya shaka, wana IT wamewatunuku shahada hii ya aina yake. Hata kama ni utani, inawasilisha picha na taswira halisi ya yaliyoko nyuma ya pazia kwa watawala wetu.

11 comments:

Malkiory Matiya said...

Hii inalipa kwa kweli! niruhusu mkuu niitundike kwenye kwenye blogu yangu ili tufikishe ujumbe huu muhimu kwa kasi.

NN Mhango said...

Mkuu Malkiory tundika tu mie sina noma. Maana wajibu wa kusambaza habari ni wetu sote kwa sawa. Sambaza tu sambaza kaka.

Anonymous said...

Ujumbe gani? Ni mijitu isiyo na akili yenye kusambaza ujumbe usio ujumbe!

Long live Dr. Kikwete!

Tafuteni zenu tuzione!

NN Mhango said...

Sisi hatutafuti kwa kugawiwa au kuhongwa. Tunazo tayari. Si vihiyo wala mazezeta wa kushabikia maangamizi kama anonymous. Jamani hata kama mnanenepeshwa kwa makapi toka kwa hawa mafisadi jitahidi muiangalie jamii kwa upana wake. Kama hali hii itaendelea hata hayo makapi mnayolishwa hamtapata fursa ya kuyafakamia. Akina Ben Ali na Mubarak na waramba viatu wao walikuwa wakifikiri kama nyinyi. Mie nadhani ni akili kuionyesha jamii aina ya watu waliowaamini ofisi zao. Mtake mchukie mpasuke hata kujinyonga hatuaacha kuwaandama mabwana zetu.

MwaJ said...

Kaka Mhango umenena. Eti long live Dr. ..........! Khaa hata aibu haoni! Hivi ameziona 'ambulence pikipiki' zilizoletwa na huyo Dr. wake? Mh! Wakati mawaziri wanajinunulia mashangingi ya mamilioni ya fedha wananchi wananunuliwa pikipiki eti za kubebea wagonjwa badala ya ambulence! Yaani hicho kitanda cha mgonjwa kilichofungwa pembeni ya pikipiki kinatosha kukuongezea ugonjwa wa moyo kwa woga utakao kuwa nao kulala hapo!

NN Mhango said...

Mwa J
Hawa wapuuzi wanaoabudia mabwana zao mafisadi wasidhani watanzania wote ni waroho kama wao au mafisi kama wao.
Kwa watu wenye akili wameishastuka kuwa hizi bajaj zitamaliza watu. We ngoja ajali za barabarani ndiyo ukweli utadhihirika. Madereva wa dala dala watazigongelea mbali wakikimbiza na foleni na pesa. Kwenye comment yangu ya juu nilimaanisha mabwana zetu yaani hawa wanaotaka tuwe mbwa mwitu na mafisi kama wao kwa kuabudia makapi.

Malkiory Matiya said...

Safari ya kuelimisha bado ni ndefu, ebu fikiria kuna mtanzania mmoja toka New York baada ya kuona hii picha kwenye blogu yangu alitoa comment ya kunikejili kama anonymous. Hajui kuwa sisi hizi gadget zingine hatujaziweka kama mapambo kwenye blogu zetu. Awali nilifikiria ni mtanzania aliyeko tz,angalau ningesema ni mmojawapo wa mafisadi au watoto wao wamejibu ni baada ya kufuatilia IP address yake ndiyo nikajua ni wa kutoka Marekani. Fikiria mtu kama huyu ambaye tunaweza kusema ameona dunia inavyozunguka anathubutu kuutetea ufisadi je mwananchi wa kawaida aliyeko kijijini?

NN Mhango said...

Kaka Matiya usishangae. Hujawahi kuona mashoga tena wenye digrii na wengine hata maprofesa? Wakati mwingine elimu au uzoefu wa mtu haundoi upumbavu wake wa kuzaliwa nao.

Usishangae saa nyingine amefika huko New york kufanya ubalozini kwa kusaidiwa na ulegelege na mfumo wa kujuana vya Kikwete.
Kwani unadhani hao mabalozi na wafanyakazi wa balozi zetu nje wanafaa zaidi ya kutokana na mitandao ya kifamilia na kichama hata rushwa?
Mie nawajua hata majaji walioteuliwa na JK lakini ukiangalia merits zao unabaki kushika tama.
Hivyo la kufanya ima ni kumtapikia au kumdharau.
Kwa vile hili linawachoma tutawachoma sana kwa kuzidi kutundika vitu kama hivi.

Malkiory Matiya said...

Mhango: Upo sawa kabisa, kuna huyu balozi wetu nchi Marekani amekuwa akipigiwa debe sana na blogu ya jamii, nilikuwa nikijiuliza hivi yeye na balozi mwenzeke aliyebadilishana naye posti kwanini wanapata publicity ya media ukilinganisha mabalozi wengine.Nilikuwa sipati jibu, awali nilidhania pengine kwasababu wapo kwenye nchi za superpower lakini nilikuwa nikitilia shaka kama hilo ndiyo jibu sahihi.

Hivi karibuni nilipata majibu ya baadhi ya maswali yangu pale niliposoma kwenye gazeti moja kichwa cha habari " BALOZI WA JK AHUSISHWA NA SCANDALI YA DOWNS) na kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti hilo kulikuwa na picha balozi wetu nchini Marekani, Mwanaidi Maajar!

Mcharia said...

Hicho cheti hakitoshi, aongezewe na kingine.

NN Mhango said...

Matiya hujakosea. Maajar ni tone katika bahari. Huyu alikuwa na ofisi yake ya uwakili maeneo ya Kariakoo akiwa wakili asiye na soko. Lakini JK alipoingia madarakani mambo yake yakanyooka. Alimfanyia nini nani anajua? Mtu mwenyewe anajulikana kipaumbele chake kwa akina mama ni nini.

Wapo wengi ima wafua nepi za ufisadi au wavua nguo kwa wakubwa kwa kuhonga miili yao wafike hapo walipo. Hivi mtu kama Hawa Ghasia zaidi ya kuwa shemeji ana sifa gani kuwa waziri? Watu kama Emanuel Nchimbi, Mary Nagu,Makongoro Mahanga, William Lukuvi na meya wa jiji la Dar Didas Masaburi wanaojulikana walivyoghushi shahada zao kama si kuwa maajenti wa mafisadi wakubwa wangekuwa bado kwenye ofisi za umma? Nani anawagusa? Ukienda Uwanja wa ndege wa JKNIA hata KIA, uhamiaji, kwenye vituo vya kukagua mafuta, TRA, THA,BoT, Utalii na mbuga za wanyama na kila sehemu inayoingiza pesa wamejaa ndugu na watoto wa mafisadi walioko serikalini. Hata wakuu wa wilaya kama Nape Nnauye, John Mongela nao wamo.Kwa ufupi ni kwamba hawa mafisadi wameiweka rehani nchi yetu. Tusipoandamana Tahrir tumekwisha.