How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Saturday, 12 March 2011
Kapayukaji katimiza nusu mwaka
Kapayukaji kanakaribia kumaliza nusu mwaka hata kama hakajapayuka. Hii ni picha yake ya sasa. Tunazidi kumshukuru Mungu azidi kukawezesha kaje kupayuka baadaye na kuchukua mikoba.
Kwa niaba ya Kapayukaji,familia, nami binafsi nawashukuruni nyote mliotutakia heri na fanaka. Naamini Mungu amesikia dua zenu na atazifanyia kazi. Kila la heri. Mungu awazidishie.
Asante kaka Mbele kuongeza dua. Ni kweli katoto kanaendelea vizuri maana kananyonya maziwa ya mama na si ma-junk au formulae. Nazidi kuwashukuru wote mliotutembelea na kutuombea heri na makuzi mema kwa kitoto chetu.
12 comments:
HONGERA sana shangazio yangu kwa kuyimza nusu mwaka. Mwenyezi Mungu na akulinde uzidi kukua na uwe na afya njema .
Tunamtakia afya njema,sina shaka naye kwa kuridhi mikoba, mwonekano wake pichani ni kielelezo tosha kuwa ni mpiganaji makini.
Napenda nirekebishe neno hapo juu: Kurithi badala ya kuridhi.
Naam. Kametulia kapayukaji ketu katarajiwa.
Kwanza kula 5, maana hapo utakapoanza utakuwa na speed ya kimbunga sababu njia imeshatengenezwa...wuuu!!!
Mwenyezi Mungu ampe afya njema awe mtoto mwenye furaha siku zote.
Napenda sana watoto.
HONGERA SANA KAPAYUKAJI NA MPAYUKAJI KWA KUWEZA KUMFIKISHA HAPO ALIPO. MAISHA NI HATUA.....
Kwa niaba ya Kapayukaji,familia, nami binafsi nawashukuruni nyote mliotutakia heri na fanaka. Naamini Mungu amesikia dua zenu na atazifanyia kazi.
Kila la heri. Mungu awazidishie.
Picha nzuri sana na katoto kanaelekea kufanana na baba yake. Kwa huu nusu mwaka kamefikia hapo, ni wazi kanaendelea vizuri. Kila la heri
Asante kaka Mbele kuongeza dua. Ni kweli katoto kanaendelea vizuri maana kananyonya maziwa ya mama na si ma-junk au formulae.
Nazidi kuwashukuru wote mliotutembelea na kutuombea heri na makuzi mema kwa kitoto chetu.
Hongera kapayukaji ketu. Kua salama. Harakati za Ukombozi zinakusubiri!
Post a Comment