Thursday, 5 February 2015

Utalii unapotangazwa kwa kutalii!

unnamedk1
Kumezuka aina mpya ya ufisadi na wizi wa fedha za umma ambapo baadhi ya wakubwa wa wizara fulani hulazimisha au kuzua safari za nje ili walipwe per diem. Kwa sasa wizara ya utalii inaongoza kwa hujuma hii ambapo wazito huenda nje kufanya upuuzi na kulipwa per diem. Mbona hatuoni wenzao wa Kenya wakifanya hivyo? Ajabu Kenya na kutotangaza utalii wake inapata watalii wengi kuliko Tanzania. Hebu angalia hiyo picha hapo juu utitiri wa walaji wakiwamo wabunge eti wanakwenda kutangaza utalii. Boresheni utalii badala ya kuibia umma kwa kizingizio cha kutangaza utalii wakati mnapiga dili.

No comments: