Monday, 16 February 2015

Sijui hili dege nalo litatuibia kiasi gani?


Baada ya mafisadi kuliua shirika la Ndege Tanzania (ATC) kumekuwa na mchezo wa kwenda nje na kukodi ndege mbovu toka kwenye makampuni ya kitapeli mojawapo likwa la Lebanon na hatimaye kukatiza mkataba na nchi kupoteza mabilioni ya fedha.Inaonekana mchezo umenoga na kukolea kiasi cha ufisadi huu kurejewa kila mara bila wahusika kuchukuliwa hatua. Tunazidiwa na viinchi vidogo kama Malawi na Rwanda wana National Carriers zao? Watanzania tumerogwa na nani kwa kuingiliwa na mdudu wa tamaa hivi? Sijui na hilo dege hapo juu litazamisha mabilioni mangapi punde si punde.

No comments: