Wednesday, 18 February 2015

Wizi na Utalii Mwingine Huu Hapa

luk4

Hapa ni ujumbe wa wazira ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukiwa kwenye matanuzi huko Singapore kwa kisingizio cha ziara ya kikazi. Kwanini ziara ya kikazi isifanyike nchini badala yake ifanyike ughaibuni kama siyo kutaka kutalii na kutafuta kulipwa per diem? Walianza wizara ya Utalii na sasa hawa wamefuatia. Kesho utaona ujumbe wa wizara nyingine nje ukitalii kwa kisingizio cha kujifunza hili na lile wakati ukweli hii ni aina mpya ya ufisadi. Nani atawazuia iwapo bosi wao mwenyewe Vasco da Gama JK ni bingwa wa jinai hii?

2 comments:

Anonymous said...

Huduma yenye kasoro lazima kitumia nguvu nyingi sana kutangaza huduma yake

Maana waliwawahi kutumia hiyo huduma wanakuwa siyo mabalozi katika kuitangaza hiyo huduma kwa sababu ni duni na dhaifu. Waswahili walisema kizuri....kibaya cha jitembeza

Sasa gharama inayotumika ni kiasi gani kutangaza utalii na kulinganisha mapato yake.

NN Mhango said...

Anon nimekuelewa japo sikubaliani na mawazo yako kuwa wanatangaza chochote.Hawa ni wezi wa kawaida wanaotumia visingizio hivi na vile kuwaibia wananchi. Hawana lolote bali kujihudumia kihalifu. Wanapaswa kufikishwa mahakamani bosi mhimili wao wa ufisadi Kikwete akiondoka mwezi Oktoba.