Thursday, 26 February 2015

Sijui Kikwete analipwa kwa nini na lipi wakati ni mzururaji?

unnamed
Kikwete akiweka shada la maua kwenye makaburi wa wendazake marais wa zamani wa Zambia Levy Mwanawasa na Fredrick Chiluba mjini Lusaka.
Juzi alikuwa nchini Kenya kwenye mkutano wa wakuuw a EAC. Kabla ya hapo alikuwa Davos. Nadhani muda anaokaa ikulu na Tanzania ni mdogo kuliko anaokaa kwenye ndege. Hakika Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais wa hovyo, dhaifu, fisadi na mzuraraji aliyewahi kutokea katika historia ya Tanzania. Laiti tungemwelewa baba wa taifa Marehemu Mwl Julius Nyerere tusingechagua hasara na sanaa kukaa ikulu kwa miaka kumi.

No comments: