The Chant of Savant

Monday 7 March 2011

Ingekuwa Ufaransa Kikwete na Mkapa wasingekufuru


Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac (78), amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za uhujumu na ufisadi kabla ya kuwa na akiwa madarakani.

Mwanzoni wanasheria walipotaka kumshitaki alijificha nyuma ya kinga. Lakini kadiri siku zilivyoyoyoma, Chirac alijikuta kweupe uso kwa uso na mkono wa sheria na aibu ya umma aliouibia.

Laiti Tanzania tungekuwa na mfumo wenye akili kama wa Ufaransa, Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa wangemalizia muda wao Segerea au Ukonnga kutokana na madudu waliyotenda wakiwa madarakani hasa Dowans, EPA, IPTL, Meremeta, Net Group Solution, SUKITA,Mwananchi Gold,Richmond, Kagoda, Kiwira, Radar na ndege ya rais, nyumba za umma,Songasna mengine mengi ambayo bado yako nyuma ya pazia. Huenda mambo yatabadilika huko tuendako. Tuombe Mungu haki itendeke bila kuangalia uso wala ukoo wa mtu. Kwa habari zaidi
, bofya hapa

2 comments:

Jaribu said...

Bado tuko na mfumo wa Ulaya during Middle Ages, ma-lords wachache na serfs. Lords can do no wrong. Until wananchi wote wanaondoa kasumba ya unyenyekevu no matter what, tutaendelea kuvumilia ufisadi wa our overlords.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu usemayo ni kweli tupu. Bado tuko kwenye karne ya Adam na Eva. Hata ile ya Yesu na Mohammad hatujabahatika kuifikia ingawa tunajisifia dini zetu. Mie huwa naona kama hatuna dini maana kukubali ufisadi ni ukafiri wa aina yake.