The Chant of Savant

Wednesday 23 March 2011

Kumbe Shehe Mkuu haoni na ni fisadi!


Mtu anaweza kuwa na jina hata wadhifa mkubwa lakini akafanya mambo madogo. Hii imejidhihirisha baada ya Shehe Mkuu Issa Simba kujitokeza hadharani na kulaani maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhamasisha wananchi kukataa ufisadi na kuboresha maisha yao.
Vikundi vingi vya kiislamu vimekuwa vikilalamika kuwa BAKWATA ni nyumba ndogo ya
CCM. Sasa ukweli umedhihirika kwa maneno ya Simba. Hivi karibuni alikaririwa akisema: “Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani,”
Kweli huyu mtu ana macho asiyeona ufisadi wa kutisha unaofanywa na serikali na CCM? Je amepofushwa nani-upendeleo wa kodi au ulinzi anaopewa na CCM?
Je maneno kama haya yalitegemewa kutolewa na mtu mwenye hadhi ya shehe mkuu? Je shehe mkuu hajui kuwa ufisadi na madhara yake havijui dini? Je CCM inashambuliwa kutokana na mwenyekiti wa kuwa mwislamu au fisadi? Huyu bwana anahitaji kuelimishwa kama huu ndiyo uwezo wake wa kufikiri kiasi cha kujipayukia bila kujali wadhifa na nafasi yake. Kwa ufupi ni kwamba shehe mkuu licha ya kujidhalilisha kwa umri na hadhi yake, ametangaza wazi alivyo shirika na mafisadi. Hana tofauti na akina Augustine Mrema, Ibrahim Lipumba, Maalim Seif Hamad na waganga njaa wengine. Je waislamu watakubali kutumiwa hivi?

11 comments:

Anonymous said...

Naona sasa unakosa heshima na kiongozi wetu wa kidini.

Anonymous said...

Mwandishi wa habari hii ni mpuuzi, hapa unaleta mapenzi na maslahi ya chadema. Ni nani asiejua kuwa chadema inaleta vurugu ktk nchi? inahatarisha amani? Pia unashangaza kwamba ati viongozi wote wa upinzani ni wanafiki ispokuwa Slaa na wenziwe wa chadema.
Wewe ni mpuuzi tu, na huna namna ya kuwasafisha chadema mbele ya jamii waonekane safi. Ni watu wenye maslahi binafsi tu, wenye kukubali damu za wengine zimwagike ili mambo yao yazidi kukaa sawa.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anonymous one na two shukrani sana kwa mawazo yenu ingawa sikubaliani nayo wala mimi si mpuuzi.
Na muelewe fujo nchini zinaletwa na mafisadi na si wanaowaandama mafisadi.
Siku shida zitokanazo na ufisadi zikiwakumba mtaelewa somo na kujilaumu. Kila la heri

Jaribu said...

Usiwajali hao, Mhango. Wananufaika na hali iliyopo sasa. Mara kiongozi wa dini, mara vurugu na uchochezi; ni kutapatapa tu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Asante Jaribu. Mtu mzima atishiwi nyao na isitoshe wanaficha majina yao kuonyesha walivyo woga na wanavyosimamia kitu cha hovyo. Hata hivyo si kosa lao-ujuzi, njaa na upogo.

Anonymous said...

Shehe mkuu ni msenge kama waislam wengine. Kwa siku wanajitia madole mara tano. Msenge ni msengi tu hata akiwa shehe mkuu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nilishawishika kuiondoa comment hiyo hapo juu lakini nikasita kutokana na watu kuwa na uhuru wa kutoa mawazo. Naonya kama matusi yataendelea, nitashindwa kuvumilia maana hakuna mwenye haki wala uhuru kuliko wengine. Tutajahidi kutumia lugha ya kistaarabu hata kama tunatofautiana kimawazo.Hakuna mwenye leseni ya kutukana wala kunyanyasa, kunyamazisha wenzake.

Anonymous said...

Iondoe kwa maslahi ya 'umma'

Anonymous said...

Mhango usiondoe hiyo comment. Kweli shehe mkuu ni msenge tu wa kawaida.

Jaribu said...

Wewe mjamaa wa juu hapo, ingawa mimi siyo mmiliki wa blog hii, unahitaji kukuza na kuimarisha ubongo wako. Kutukana watu kwenye blog siyo ujanja, any idiot can do it.

Anonymous said...

sidhani kama shida ya maji,barabara,umeme,bei za vitu kupanda hovyo n.k ni mambo yanayotaka dini flani iyatete maake wote tu mumo sifani,...anyway hasira za wananchi si dhidi ya uislam au ukristo wala din yoyote ile ila ni juu ya mfumo wa utendaji kazi wa serikari iliyopo madarakan....waache kugawa watu wa udini wao