Saturday, 27 September 2014

Ukishindwa kufanya kazi ardhini fanyia angani

 Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye ndege yake. Anaonekana anasaini nyaraka. Wapo wanaoona kama mkwara tu, anatanua kama kawaida yake. Kimsingi, kwa waswahili hakuna lisilo na jibu. Ukiuliza inakuwaje rais hakai ofisini utajibiwa kuwa ukishindwa kufanya kazi ardhini basi unaweza kufanyia angani. Nani anajali iwapo wanaolipia mafuta ya dege ni wale wale waliopigika? Huyu ndiye rais kipenzi cha watu anayeweza kuwatumia atakavyo kwa vile wanampenda naye anawapenda. Lazima hapa yawepo mapenzi ya kimshumaa.
Sina ugomvi na utanuaji wa Kikwete. Tabu yangu siku zote ni ile hali ya kuficha wale anaoandamana nao utadhani kuna soo! Au kuna watu wasiopaswa kwenda kutanua kwa njuluku za umma wanaopenyezwa kwenye msafara wa bwana mkubwa ambao umegeuka kuwa top national security agenda?

2 comments:

Anonymous said...

khakhakha!!

NN Mhango said...

Anon kwanini unacheka?