The Chant of Savant

Saturday 14 February 2015

Yakhe mwatangaza utalii au mwatalii wenyewe?

Juzi nikiwa nakamata kanywaji baada ya kupiga mibangi si bim kubwa wangu akanipa inshu moja kali. Kwanza, nikiri, pamoja na ubingwa wangu wa udaku, hii ilikuwa imenipiga chenga tokana na kuutwika sana ili kuondoa mawazo ya kuambiwa kuwa nishiriki kwenye uharamia wa kuua kaya yaani kupiga kula ya kura kwenye kupitisha katiba mizengwe. Nikiwa sina hili wala lile si bi mkubwa akanitonya kuwa kuna ka mchezo ka ulaji kameanzishwa na wajanja fulani kwenye wizara moja ya utalii. Jamaa anasema tena hawa wanjanja wanapohujumu kaya kwa kutalii wakijifanya wanatangaza utalii hawana wasiwasi. Watakuwa na wasiwasi gani kwenye kaya ambamo ufisadi na wizi wa fedha za wanuka umaskini unalipa? Wataogopa nini iwapo wametungiwa hata katiba ya kuwalinda kwa kuinyotoa roho rasimu mardadi ya jaji Wariobha? Who cares if paupers are pauperized even more? Naongea kimombo ili kuonyesha kuwa sikughushi kama wale madingi waliokingia kifua na dingi mkuu wakijiita madaktari wakati si lolote wala chochote bali madakichari?
          FYI – kwa wasiojua FYI –maana yake ni For Your Information, kumezuka aina mpya ya ufisadi na wizi wa fedha za umma ambapo baadhi ya wakubwa wa wizara fulani hulazimisha au kuzua safari za nje ili walipwe per diem. Kibaya zaidi hawaendi wawili wala watatu. Inaenda mob kubwa tu ya walaji na wasaka posho na kukaa huko tena kwenye mahoteli ya bei mbaya kwa miezi siyo siku wala wiki. Kimsingi, unakwenda ukoo mzima wa walaji mamboleo waliojazana kwenye ofisi za kaya wakihomola kana kwamba ni shamba la bibi.  Kwa sasa wizara ya utalii inaongoza kwa ka mchezo haka ambapo wazito huenda nje kufanya upuuzi na kulipwa per diem. Mbona hatuoni wenzao wa Kenya wakifanya hivyo? Ajabu Kenya na kutotangaza utalii wake kupitia utalii wa wakubwa wa wizara yake, bado inapata watalii wengi kuliko Danganyika aka Bongolalaland. Hali ni mbaya. Hata wahishiwa nao wanahadaiwa na kulala kitanda kimoja na wezi wa njuluku za umma wa wachovu bila huruma wala kugutuka!
          Boresheni utalii badala ya kuibia umma kwa kizingizio cha kutangaza utalii wakati mnapiga dili na kutalii nyinyi wenyewe badala ya kuacha watalii waje watalii. Kama utalii wenyewe ni huu heri tusiwe na watalii. Maana ukiangalia gharama za wakubwa zetu kwenda kutalii ulaya na Marekani si ajabu zikawa kubwa kuliko hiyo njuluku wanayoleta watalii nayo ikiashia kuibiwa na akina escrow, Richmonduli, Kagoda na majizi mengine yaliyotamalaki kayani.
          Utasikia ujumbe wa kutangaza utalii kwa njia ya kutalii uko Hong Kong, mwingine New York, na mwingine London na miji mingine mikuu ya majuu. Mwatangaza utalii au mwatalii kwa kisingizio cha kutangaza utalii?  Mbona hatuwaoni Kigoma, Likawage, Isingiro, Ibadakuri, Mlola, Mlalo, Mtae, Nguriati, Ngudu au Matemanga? Kwani wabongo hawawezi kutalii ndani ya kaya yao? Narudia, mnachofanya ni kutangaza utalii au kutumia kutangaza utalii kutalii?
          Baada ya kuinyaka hii ya utalii wa kutalii kwa kutangaza na kutumbua, niligundua wizara nyingine ambayo ni ya njuluku ambayo wakubwa zake huenda zao Washington kwa Joji Kichaka eti kujadiliana na World Bank na IMF wakati uchumi wao ni mfu kutokana na wao kuendekeza ufisadi. Juzi si mlisikia wenyewe kuwa na Takokuru iliyopewa jukumu la kupambana na rushwa inaupamba na kuushiriki. Nilimsikia mwenyewe kwa masikio yangu na kumuona kwa maninga yangu mkubwa wao Dk Eddie wa Shea Hoshea akikiri kuwa yeye na watu wake wanakwanyua rushua. Kama wanakula rushua wanangoja nini kwenye ofisi za umma tena wakilipwa njuluku kibao.         Huwa siachi kujiuliza: Kama majambazi kama escrow Rugemalayer na Seti Singsong wanawashinda, mnadhani kwenda IMF na WB kutakuza uchumi wetu? Kama hampunzi ziara za wakubwa na wadogo kwenye ulaji mnadhani uchumi utakuwa? Akili gani hii? Hata bibi wa bibi yangu alikuwa mchumi mzuri kuliko wao. Kwa sababu alijua kuwa ukitumia kuliko unavyopata unaishia kufilisika. Hii ndiyo Danganyika. Mnaacha Tanzanite zinafaidiwa na Kenya na India mnadhani mtasonga mbele. Twiga mnauza uarabuni huku tembo wakiteketea mkipakia meno yao hata kwenye ndege za wanene wa Uchina halafu mtegemee kuendelea? Akili au matope? Shame on you all fisadis regardless you are big or small. Mshindwe na kunyong’onyea kabla ya kuteketea kwa miwaya na pressure ya moyo.
          Mlevi mmoja aliniacha hoi baada ya kusema eti mkuu anapaswa kuzuia jinai hii. Kwa vile alikuwa ameutwika mma nilimuonea huruma. Sikumkata mabao. Maana,kama walevi na wachovu wote wanawaza hivi, basi tumekwisha. Nani amzuie nani wakati nyani wote huiba mahindi? Utalii si kutangaza utalii tu bali hata kuombaomba, kukopakopa, kuhudhuria mikutano isiyo kichwa na miguu kama ule wa Davos ambapo wenye nazo hukutana kujadili mafanikio yao. Ajabu utaona na viranja wa kaya kapuku kichwakichwa kila mwaka kwenda kuhudhuria. Ukiwauliza kuhudhuria kwao kumebadili nini wakati kaya zao zinaendelea kuwa apeche alolo wakati wao wakizidi Umatonya, wanatoa mimacho kama bundi aliyefumwa mtegoni asubuhi. Watabadili nini iwapo wanashindwa kupambana na mafisi na mafisadi kayani mwao? Kwani hawapo na hamuwajui au woga na unafiki tu. Mie sijali. Nikishapiga mibangi yangu simuonei ngurumbili huru wala simuangalii nyani usoni. They can all go to hell so that we can have competent constitution and leaders not robbers. Ohoo! Wajua nini? Ukitaka kuongea ung’eng’e kata kalaji. Haya ninayoandika leo ukiniuliza baada ya mibangi na kanywaji kunitoa lazima niite jamaa yangu aitwaye Dictionary d/o Kamusi.

          Tumalize kwa kulaani utalii wa kutangaza utalii wakati kwa lugha sahihi ni wizi, ufisadi, uzembe, uzururaji, uhujumu, ujambarika! We stop! Salamu kwa Lazio Nyalaaanduuuu!
Chanzo: Nipashe Feb,. 14, 2015.

4 comments:

Anonymous said...

Tena inashangaza kuna kijibalozi mdogo Dubai huyu mtoto si mtanzania mama ni mkenya na anaishi Kenya licha ya yeye kusoma Tanzania, huyu ndo fisadi no 1 kwani ndo wakubwa wote hutorosha fedha zetu na kupeleka Dubai, inashangaza sana kupewa nafasi nyeti wakati si mtanzania huyu, na mkewe anafanya kazi benki Dubai kila wiki yupo bongo kutorosha madola kupeleka Dubai , kisa rafiki wa Membe

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umenena. Mwaga detail huyu mwizi na fisadi afichuke.Siku hizi nchi za kiarabu zimeiweka kati hata kuliko zama za utumwa. Ipo siku yote yatafichuka. Nadhani ghuba ni sehemu maalum kwa Bongo ikizingatiwa hata ile nyumba ndogo ya bwana mkubwa ambayo imefichwa baada ya kuiandama iko huko. Mwamkumbuka Rahma Kharoos? Amefichwa wapi siku hizi?

Anonymous said...

Kinapenda sana sifa hichi kibalozi mchwara kila kukicha mtaandaoni na kutangaza eti wawekezaji,atawafutia watu kazi Dubai, wizani hatumpendi sana huyu , lakini tufanyeje anakula na wakubwa waziri na rais
Lakini yote yanamwisho 2015

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Unasema Omar Mjenga siyo? Zake zinahesabika na yote yatajulikana siku si nyingi.