Wednesday, 30 September 2015

Kamanda Nkuzi alivyosherehekea Birthday yake
Kamanda wetu Nkuzi alitimiza miaka mitano sambamba na kuanza vidudu huku mdogo wake kama Nkwazi Jr akitimiza miaka mitatu wakati dada yao Mkubwa Nthethe alianza chuo kikuu mwezi huo huo. Tulisheherekea tulivyoweza kwa kutoka nje kidogo. 

3 comments:

Anonymous said...

Hongera Mwalimu na familia yako bora!!!, isiyoishi na kusoma, kuendesha shughuli za maisha bila ya kutumia fedha za kifisadi. Huku kwetu sisi ukiweza kumudu gharama za huduma kwa watoto namna hiyo basi tegemea zimewezekana kwa sababu kuwaibia wa walalahoi haki zao na pesa zao. Na itakuwa kwa namna tano tuu za uhalifu wa silaha au kuwa kiongozi mwizi wa umma au mfanyabiashara mkwepa kodi au kuhua tembo au kusafirisha wanyama hai ughaibuni hususani nchi za mashariki ya kati.

Na wakati wa kuwachagua tena wanakuja kututukana na kutuita malofa na wapumbavu kwa sababu tunastaili kuitwa hivyo kutokana kudumaha kwa akili zetu kwa sababu lishe duni, elimu duni, huduma za afya duni, maarifa duni, nk

Yasinta Ngonyani said...

Hongera nyingi sana kwanza kwa wazazi/walezi kwa malezi. Na Hongera sana Kamanda Nkuzi kwa kutimiza miaka mitano na sasa nakupa maneno haya uwe kijana mtii kwa watu wote katika dunia hii pia soma kwa makini...HONGERA SANA..SHANGAZIO Yasinta/Kapulya.

NN Mhango said...

Anon na da Yasinta nawashukuru kwa salamu zenu tamu. Tunajitahidi kuendelea kupambana na maisha kihalali. Nakubaliana na Anon kuwa tunalea watoto kihalali. Uzoefu unaonyesha kuwa watoto wanaolelewa kwa fedha za kifisadi wakati mwingine hutokea kulipia vibaya kama ilivyotokeea kwa watoto wa Gaddafi na Saddam bila kumsahau Mubarak. Hata hawa mafisadi wetu kuna siku wao ama watoto wao watalipia. Da Yasinta ujumbe wako nimeufikisha kwa mwanao Nkuzi. Nawatakieni kila la heri na kuzidi kuwakaribisha ugani.