Thursday, 3 September 2015

Rais aswekwa lupango


Rais wa zamani wa Guatemala, Otto Perez Molina amesweka rumande akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa toka kwa wafanyabiashara ili wakwepe kodi. Baada ya kukumbwa na vuguvugu la umma la kumtaka ajiuzulu na kuwajibika, Molina alilazimika kujiuzulu baada ya kujaribu bila mafanikio. Alijaribu kuwatoa kafala mawaziri wake watatu bila mafanikio. Alimtoa kafala makamu wake wa rais wa zamani bila mafanikio. Umma ulishikilia uzi ule ule hadi akaachia ngazi kwa aibu. Angekuwa rais wa kiafrika hasa Tanzania wala asingeondoka wala kuhangaika. Hata kama angeondoka asingelala lupango. 
Molina kuanzia leo anaonja joto ya jiwe kwa kulala rumande akingoja kusomewa mashtaka yahusianayo na ufisadi. Baada ya kuporomoka kwa Molina, makamu wake wa rais Alejandro Maldonaldo  aliapishwa kuhudumu kama rais wa mpito hadi uchaguzi utakapofanyika. Kwa mara nyingine nguvu na vuguvugu vya umma vimeangusha mbuyu.

No comments: