Wednesday, 12 November 2014

Kashfa rais wa China kusafirisha vipusa ikulu ijilaume yenyewe

 
KASHFA ya ndege ya Rais wa China, Xi Jinping kusafirisha pembe za ndovu haikushangaza wengi. Wengi walitegemea hili hasa kutokana na mambo yanavyofanya nchini. Baada ya vyombo mbali mbali vya habari duniani kuripoti kuwa ndege yake ilisafirisha maelfu ya kilo za pembe za ndovu alipofaya ziara nchini hapo, Machi mwaka jana, japo zilichelewa, zina funzo kubwa kwa watwala wetu.
Baada ya taarifa kusambaa kila mahali, serikali ilijitoa kimasomaso kukanusha kwa majibu yenye utata. Majibu ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe yaliacha utata badala ya kusafisha hewa. Membe alikaririwa akiliambia Bunge kuwa madai ya ndege ya Rais kusafirisha pembe za ndovu ni wivu wa washindani katika biashara.
Biashara ganiMembe alisema, “Wasambazi wa taarifa hizi hawaitakii mema nchi yetu, hawawatakii mema marafiki zetu China, wamejawa na vivu na husda kwa mafanikio ya China. Inashangaza kuona wanawachukia huku wanawategemea.”
Inaonekana hawa watu wanajuana. Kwanini waziri hakuwataja hawa wenye wivu wa mafanikio ya TanzaniaKwetu sisi ndege ya Rais isafirishe au isisafirishe pembe za ndovu si hoja. Ila kwa ofisi kama ya Rais na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutuhumiwa au kuhusishwa na uchafu huu ni ushahidi kuwa taasisi husika ni za hovyo.
Kaisari aliwahi kuletewa tuhuma dhidi ya mkewe. Mkewe alikana kila kitu. Kaisari alimwambia, “Caesar’s wife must be above suspicion.” Yaani mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa vinginevyo awe amejiachia kiasi cha kuwa wa hovyo hadi akatuhumiwa. Kwa Kaisari hoja haikuwa ni ima mkewe ametenda kosa au la. Hoja ilikuwa ni usafi wa taasisi yaani mke wa Kaisari. Je, taasisi zetu ziko hivi?
Swali la kujiuliza ni kwanini hawa “wabaya na wenye wivu” wameamua kutumia taasisi nyeti kama IkuluJibu ni rahisi. Kama tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani, wanaoandamana naye kwenye ziara zake nje hawatajwi kama tulivyozea, unategemea niniJe, ni kwanini majina ya wanaoandamana na Rais yanafanywa siri?
Je, kuna watu wasiostahiki wanaopenyezwa kwenye misafara ya RaisJe, Kikwete au wasaidizi wake hawajawahi kusikia malalamiko dhidhi ya tabia hii yenye kutia shakaJe wamechukua hatua gani na wanaficha nini kama hakuna jamboImefikia mahali watu wanakwenda na Rais kupiga picha na kujidai kwenye mitandao na hakuna anayewaondoa kwenye misafara ya rais.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuonya kuwa Ikulu imegeuzwa pango la wezi. Ni bahati mbaya hata mwalimu aliporusha madai haya hakuna aliyekanusha wala kujibu hii ikimaanisha kuwa ni kweli Ikulu imegeuzwa pango la wezi.
Baya zaidi, hakuna hata aliyejaribu kurekebisha hali hii yaani kuifanya Ikulu iwe Patakatifa pa Patakatifu kama ilivyokuwa wakati wake. Watu wenye kutia kila aina ya shaka waliweza kuikalia na kuifuja.
Sasa Ikulu ikifikia hatua hii unategemea niniJe, Ikulu yetu ni safiYawezaje kuwa safi wakati hata mke wa Kaisari anafanya biashara ya NGOYawezaje kuwa safi wakati wasemaji wake wanajulikana walivyotumika kama nepi kwenye uchaguzi wa mwaka 2005Yawezaje kuwa safi wakati uteuzi inaoufanya unatia shakaYawezaje kuwa safi wakati matumizi yake yanatia shaka?
Kitu kingine kinachoweza kuwashawishi, “wabaya wetu” kutuchafua ni ile hali ya kuwa tumekubali kujichafua wenyewe. Wanajua udhaifu wetu. Na wameamua kuutumia vilivyo. Tumenasa.
Ukiachia mbali ya uhohehahe wa taasisi zetu, Rais amewahi kuguswa na kashfa mbali mbali mojawapo ikiwa kashfa ya EPA ambayo hakuikanusha wala kuwahi kuongelea. Je, kwanini Rais aliamua kukaa kimya asijitetee wakati ni bingwa wa kufanya hivyo kama hakuna ukweliNadhani badala ya kulaumu wabaya wetu wa kuchongwa, tunapaswa kujilaumu wenyewe na jinsi tunavyopata Rais na jinsi viongozi wetu wanavyofanya mambo yao. Wameshindwa hata kutaja mali zao.
Tanzania imekuwa nchi ya kashfa. Nani mara hii amesahau kashfa ya fedha ya Escrew iliyoigusa serikali yote bado inafanyiwa mizaha na mizengwe. Nani anawashughulikia watuhumiwaMbona wengi wa watuhumiwa bado wamo kwenye nafasi nyeti wakitanua kana kwamba walichofanya ni halaliJe, imekuwaje Rais asiwahusishe kama siyo mnufaika wa kashfa husika?
Msururu wa kashfa unaendelea. Rejea kashfa ya kuficha fedha nje ambayo iliibua vimbwanga pale Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alipofikia hata kumtishia Balozi wa Uswisi nchini Olivier Chave baada ya balozi kudai kuwa serikali ya Tanzania haiwapi ushirikiano kurejesha fedha husika.
Nani anaongelea kashfa hii tena wakati watuhumiwa wakubwa ndiyo hao wanapewa nafasi nyeti kama kuandika katiba mpyaJe, kwa uhovyo huu “wabaya wetu” watashindwa kutufichua sisi tukisema wanatuchafua wakati tumejichafua wenyewe?
Tukio jingine linaloweza kuonyesha kuwa tumejichafua wenyewe ni la kuteuliwa kwa baadhi ya watuhumiwa wa kusafirisha pembe za ndovu kwenye nafasi nyeti mfano Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa Cha Cha Mapinduzi (CCM).
Ina maana Kikwete hajui tuhuma hiziJe, alitumia vigezo gani kumteua mtu mwenye doa kama huyu kama hakuna namnaHivi kikitokea chombo cha habari kikamshutumu Kinana tutasema tunachafuliwa au tumehiari kujichafua?
Tanzania haina haya ya kulalamika kuwa inachafuliwa. Imejichafua yenyewe baada ya kuzika maadili ya utumishi wa umma na kuanzisha madili ya utumiaji taasisi za umma. Na bado. Vinginevyo wahusika wakubali kubadilika.
Chanzo: Tanzania Daima leo Jumatano

No comments: