Monday, 17 November 2014

Kumbe na wanasiasa wanatapeliwa!


Askofu wa kujipachika wa dhehebu la Good News for All Ministry  Charles Gadi wa pili kulia pamoja na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi kwenye maombi ya kumwombea rais Jakaya Kikwete anayetibiwa nchini Marekani baada ya kupasuliwa busha (Picha kwa hisani ya IPPmedia).

Wanasiasa huwatapeli wananchi. Kadhalika nao hutapeliwa na waganga wa kienyeji na wachunaji waitwao wachungaji. Huu mchezo umeanza kuota mizizi ambapo unasikia matapeli eti wakiliombea taifa badala ya kuliambia kuwa linaharibiwa na hawa miungu watu wanaowaabudia ili wawape tenda na vijipesa kidogo au kujifanya hawaoni utapeli wanaofanya hadi wengi wametokea kuwa mabilionea hata wanaoweza kununua ndege.
Matapeli hawa kiroho kwa kujua kuwa watawala wetu ni wachafu, woga na wasiojiamini, wamewaingiza mjini kiasi cha kuwatumia kupata umaarufu na kuwaibia. Rais wa zamani wa Malawi alitumiwa vilivyo na tapeli la kinigeria TB Joshua ambaye hata hivyo utapeli wake ulipata pigo hivi karibuni pale nyumba yake ya kulala wageni ilipoporomoka na kuua zaidi ya watu 100 wengi wakitokea Afrika Kusini ambako tapeli huyu ana wafuasi wengi.


No comments: