Thursday, 6 November 2014

Uteuzi wa Kikwete ulioniacha hoi!

Halima Dendego ambaye elimu yake ni utata mtupu kiapishwa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Mtwara
Mwantumu Mahiza mwalimu wa shule ya msingi kama Salma Kikwete aliyetueliwa muda mrefu kuwa mkuu wa mkoa
Mwanaidi Majaar mama aliyetuhumiwa kusaidia wizi wa EPA aliteuliwa balozi na hatimaye ulaji mwingine kama kulipwa fadhila. Je Kikwete ana nni na wanawake hawa? Mbona wamepanda haraka haraka wakati hawana sifa hata robo kwa walio wengi. Na hawa ni tone la maji kwenye bahari ya nyangumi Kikwete

Kwa wanaofuatilia uteuzi wa Kikwete wa watu wa kushika nafasi mbali mbali, watakubaliana nasi kuwa kuna udini, kujuana, ushikaji hata uhawala kwenye uteuzi wake. Ukiangalia wakuu wa mikoa, wilaya, mawaziri, wabunge wa kuteliwa, majaji na walaji wengine utagundua hili. Ni balaa. Utumishi wa umma umegeuzwa biashara ya kuhongana ulaji na kulipana fadhila.

No comments: