Sunday, 9 November 2014

Ugogoro wa afya ya Kikwete tunafichwa nini?

Kikwete akiongea na dk Bingwa wa upasuaji kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji
Taarifa tulizo nazo toka kwenye mitandao ya rais Jakaya Kikwete na si kwenye magazeti ya serikali ni kwamba rais anaumwa. Anasumbuliwa na kinachoonekana kuwa kansa ya kizazi. Maana taarifa zinasema amepasuliwa tezi dume (Prostate).
Kuumwa ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu ila kwa watawala wetu ambao wanajiona si wanadamu hii si saizi yao hadi yawakute ya kuwakuta. Tulidhani wangejifunza tokana na kifo cha baba wa taifa Mwl Julius Nyerere ambaye wasaidizi wake waliufanya ugonjwa wake National Security's top secret.
Hivi karibuni taifa jirani la Zambia lilimpoteza rais wake Michael Chilufya Sata baada ya kuficha ugonjwa wake kwa muda mrefu. Kinachoshangaza ni ile hali ya taarifa za ugonjwa wa rais kutolewa kwenye mitandao na kwa lugha nyepesi bila kueleza hata historia ya masahibu yake. Tunamtakia siha njema apone haraka ila tunawalaumu wasaidizi wake kuficha ugonjwa. Mficha maradhi kilio humfichua. Tusingeomba haya yaikute Tanzania. Maana kwa wanaojua historia ya ziara za mara kwa mara za Kikwete nje ni kwamba anaumwa sana tu. Wapo wanaoamini kuwa ziara za Kikwete huku na kule ni kupambana na gonjwa ambalo hataki kuliweka wazi.

No comments: