Sunday, 30 November 2014

Kikwete azidi kuwatoa kafara wenzake akiendelea kutesaUamuzi wa Bunge kuwashughulikia mawaziri na wabunge wachache ni pigo kwa uwajibikaji tanzania. kwa mara nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wamefanikiwa kuwaingiza mkenge watanzania wakiongozwa na wapizani. Nani alitegemea kuwa wangerudia upuuzi wa Richmond ambapo serikali ilipaswa kufurushwa lakini ikamtoa waziri wake mkuu kafara na kunusurika huku wakubwa zake wakiendelea kupunga madili mengine? Katika kashfa ya escrow serikali na CCM wameshinda kile waingereza huita to win big. Wameweza kutoa kafara ya kuku (mawaziri) badala ya  mbuzi (waziri mkuu) ili kumnusuru ng'ombe yaani rais. Hivyo, KIDUMU CHAMA CHA MAFISADI. Na UFISADI unaendelea kama kawa. Tuombe Mungu aingilie kati kama alivyoonyesha kwenye gonjwa walilokuwa wakificha hivi karibuni ambapo rais amekiri kuwa anasumbuliwa na kansa ya kizazi. Tuombe Mungu atusaidie kuwafyeka majambazi wetu wenye ulaji. Amin.

No comments: