Monday, 29 April 2013

Alex Massawe: Matajiri Uchwara, siasa za kijambazi na jinai


Taarifa za kukamatwa kwa mfanyabiashara mashuhuri lakini mwenye kutia mashaka nchini zinatufungua macho. Habari zilizokaririwa na vyombo vya habari ni kwamba Massawe alikamatwa nchini Afrika Kusini kutokana na makosa ambayo polisi wa Tanzania hawakuwa wazi kuyaeleza.
Massawe mwenye mrorongo wa biashara alisifika sana alipoakamatwa miaka ya karibuni akihusishwa na kufadhili ujambazi mbali mbali nchini. Tokana na ukweli kuwa Massawe ni mmojawapo wa wafadhili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesi na kashfa hii ya aina yake ilizimwa kinamna ingawa wachambuzi tulishapata ukweli. Kukamatwa kwa Massawe na majambazi wengine wakubwa kulitokea baada ya rais Jakaya Kikwete kujigamba kuwa anawajua majambazi wakubwa wote, wauza unga, wezi bandarini, mafisadi na wengine kutokana na kuwa na orodha yao. Wengi wasiojua mchezo mzima wanaendelea kuuuliza: Kama Kikwete hanufaiki na utajiri huu uchwara utokanao na jinai anakuwaje mgumu kuwakamata wahusika? Wanaouliza swali hili wanasahau kuwa bila ujambazi wa EPA na ule wa kuwachafua wengine huenda Kikwete asingekuwa madarakani! Hapa sijui ni jambazi gani amkamate nani. Mungu siku zote hamfichi mnafiki. Baada ya kulindana kwenye ujambazi wao sasa wanaanza kuuana wao kwa wao kutokana na laana ya kuwaibia watanzania maskini. Hata polisi washikwe kigugumizi juu ya maendeleo haya mapya ya  kuumbuka kwa majambazi, umma utajua tu. Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

No comments: