Tuesday, 16 April 2013

Wajue maadui wakubwa wa taifa la Tanzania


Hivi karibuni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliamua kuwaanika magaidi wa kitanzania wanaolindwa na serikali ambayo nayo inaonekana kuwa ya kigaidi. Hii ni baada ya CCM ikishirikiana na Usalama wa Taifa ambao umegeuka kuwa Uhasama na Zahama ya Taifa kutengeneza video iliyolenga kukionyesha CHADEMA kama chama cha kigaidi. Ni bahati nzuri kuwa CHADEMA walistukia mchezo mzima na kuamua kuanika ukweli. Kitendo cha CHADEMA licha ya kuwa cha kizalendo, kimeufungua macho umma wa watanzania wanaojali kuwa kumbe wanatawaliwa na genge la waharifu na magaidi wanaojificha nyuma ya madaraka ya umma. Kwa mfano, tumejua ni kwanini shutuma za kughushi zinazowakabili baadhi ya mawaziri, wabunge na mabalozi hazishughulikiwi.
Vinara wa ugaidi huu ni waziri wa Mambo ya Ndani Emanuel Nchimbi anayedaiwa kughushi shahada ya udaktari na Naibu Katibu mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba anayetuhumiwa kutumia jina la mtu mwingine kuweza kusoma sekondari. Je watanzania wataendelea na ukondoo wa kujifanya hayawahusu wakati yanawaumiza vibaya?Kwa habari zaidi BOFYA hapa uone na kusikia mkanda mzima kama ulivyoanikwa na CHADEMA.

No comments: