Sunday, 14 April 2013

Tanzania imebakwa na CCM na vikaragozi na vinyamkera wake

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewashika pabaya baadhi ya vigogo wa serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vikaragosi vyao wanavyotumia toka Usalama wa Taifa (TISS) ambayo imegeuzwa nyumba ndogo ya CCM kiasi cha kutumiwa kufanya karibu kila uchafu wa kuhujumu upinzani. Katika kashfa hii itokanayo na kutekwa na kuumizwa kwa mhariri wa magazeti ya Habari Corporation (2006) na mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Absalom Kibanda wamo wengi usiotegemea kama waziri wa mambo ya ndani, mtoto wa rais na mahabithi wengine wanaojificha nyuma ya kazi mbali mbali kama kupiga picha Ikulu na upuuzi mwingine. Moja ya jambo ambalo limetufungua macho ni kugundua ni kwanini waziri wa  mambo ya ndani Emanuel Nchimbi anayetuhumiwa na kosa  la kughushi vyeti vya kitaaluma hafukuzwi wala kuwajibishwa. Kwa ufupi ni kwamba taifa letu limebakwa na vinyamkera wasioangalia kesho kutatokea nini. Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

No comments: