Wednesday, 24 April 2013

Ghorofa laporomoka Bangladesh na kuua zaidi ya 80


Wakati watanzania wakionekana kusahau na kusuasua juu ya kuporomoka kwa ghorofa la mtaa wa Indira Gandhi, huko bara Hindi mambo yanazidi kuwa magumu. Mjini Dhakar nchini Bangladeshi limeporomoka na kuua zaidi ya watu 80. Blogu hii iliwahi kuuliza uhusiano wa kuporomoka kwa ghorofa la Dar es Salaam na yale ya India. Ukiangalia mmilki wa ghorofa lililoanguka na lile linalopaswa kubomolewa anatoka huko huko. Je Tanzania na Afrika kwa ujumla inaanza kuingiza ustaarabu wa kishenzi wa ujenzi hatari kama ilivyo huko bara Hindi? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: