Monday, 29 April 2013

Nani ataibuka mshindi kati ya watumishi hawa wa mafisadi?


Hakuna ubishi. Kuna mgogoro unarindima ndani ya Chama Cha Mapiduzi tangu lilipoporomoka jengo la ghorofa 16 kwenye mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar ambapo makundi ya kifisadi yanagombea maslahi binafsi. Kwa anayejua jinsi wafanyabiashara fisadi na hatari wa kihindi wanavyowatumia watawala wetu kama nepi, atajua ninachomaanisha hapa. 
Hakuna jambo limenishangaza kama kusoma taarifa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar Said Mecky Sadik anangojea matokeo ya tume ya uchunguzi wa kuporomoka wa jengo hasa baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kutoa agizo jengo jingine kama lile karibu na lile liloporomoka yote yakimilkiwa na mpuuzi mmoja. Kwanini kungoja ripoti ya tume ilhali chanzo cha mkasa huu kinafahamika? Yaani mara hii wamesahau hata maneno ya mlinzi jirani na eneo lile aliyewaambia wajenzi baada ya kushuhudia wakifanya vitu vya kipuuzi kuwa walivyokuwa wakifanya siyo? Hivi inahitaji tume na ripoti kujua kuwa mejengo husika yalijengwa kinyume cha sheria viwango na taratibu? Je kinachofanyika hapa si ufisadi mwingine wa kuokoa mwingine ni nini? Je Sadik anadhani watanzania wote ni mataahira kama yeye anavyetumiwa kama nepi? Je katika kipute hiki nani ataibuka mshindi kati ya hawa watumishi wawili wa mafisadi ambapo mmoja anatumikia wahindi na mwingine serikali fisadi? Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

No comments: