Friday, 19 April 2013

Polisi wakamata rais wa zamaniKiongozi wa zamani wa Pakistan Parvez Musharraf alikamatwa jana  usiku nyumbani kwake nje kidogo ya mji mkuu Karachi. Musharraf anakabiliwa na mashitaka ya uhaini yaotkanayo na kusimamisha katiba ya nchi alipochukua madaraka kwa njia ya kupindua serikali mwaka 2001. Alitawala hadi 2008 kabla ya kuachia madaraka kukimbilia Uingereza ambako alikaa uhamishoni hadi aliporejea hivi karibuni akitaka kurejea kwenye siasa bila mafanikio. Kwa mwaka huu Musharraf anakuwa rais wa pili kukamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka baada ya rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda ambaye hivi karibuni alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Kukamatwa kwa watawala hawa wa zamani ni somo kwa watawala wa sasa wanaotumia madaraka vibaya bila kujua kuwa kuna siku yatawaponyoka na wataonja joto ya jiwe. Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

No comments: