Wednesday, 24 April 2013

Tuwaunge mkono wakulima wa korosho walioamua kujikomboa


Si siri tena kuwa kondoo ameamka kiasi cha kumtembezea fisi mateke! Ingawa wakulima wa Tanzania wamekuwa wakitumika kama mtaji mkubwa wa kukiweka Chama Cha Mafisadi (CCM) madarakani, upepo umeanza kubadili. Hivi karibuni huko mkoani Lindi wakuliwa wa korosho waliamua liwalo na liwe. Waliamua kusema kwa herufu kubwa ENOUGH IS ENOUGH. Vurugu zilitokea na nyumba kuchomwa moto huku serikali ikikirika kuwakamata iliowaita wachochezi wakati ni wapigania haki na ukombozi wa kweli. Hakika yale niliyoandika kwenye kitabu changu ambacho hata hivyo hakijapokelewa vizuri na watawala cha SAA YA UKOMBOZI yanaanza kutumia nikiwa kijana bado. Namshukuru Mungu na kuzidi kuhanikiza nikiwataka watanzania kusimama kidete na kidedea kuhakikisha tunawaondoa hawa nunda wala watu na manyang'au walitukalia kooni kwa muda mrefu. Inafurahisha kuwa habari hii sasa inaanza kupiga hodi kwenye vyombo vya kimataifa. SAA YA UKOMBOZI IMEWADIA TUSIMAME NA KUJIKOMBOA.
Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

No comments: