Sunday, 21 April 2013

Hekalu la Rwakatare lazidi kuitesa serikali

 Hekalu hili la bei mbaya lilipozinduliwa na Getrude Rwakatare aliyejipachika uchungaji wanaojua jinsi dini zinavyotumika ima kuwaibia maskini au kuficha biashara haramu walihoji. Baadaye zilitoka habari kuwa limejengwa kwenye eneo lisiloruhusiwa kisheria hivyo kupaswa kuvunjwa sawa na wengine waliokuwa wamejenga kwenye eneo husika ambalo ni mkondo wa bahari. Hivi karibuni sakata hili limeibukia bungeni ambako mbunge wa viti maalumu Esther Bulaya (CCM) aliamua kulivalia njuga. Wenye kufuatilia tunangojea kuona hili suala litapigwa dana dana hadi lini. Sambamba na hili tunangojea kuona lile jengo la gharofa 16 la Mtaa wa Indira Gandhi lililoamriwa na waziri Anna Tibaijuka kubomolewa litabomolewa lini. Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

No comments: