Saturday, 26 April 2014

Are these actors serious at all?Kwa wanaojua jinsi Jakaya Kikwete anavyomchukia Nyerere na jinsi alivyomuangusha wanashangaa kuona haya mapenzi ya ghafla bi vu. Wawili hawa walivyoshika picha za waasisi wa muungano utadhani wanawapenda zaidi ya kupenda ulaji na ajenda zao. Tangu lini Kikwete aliyekataliwa ulaji na mwalimu akampenda zaidi ya kumponda? Wameishiwa hadi wanatumia wafu pale waliposhindwa kujitetea. Ni aibu na unafiki kiasi gani? Kama kuna watu wanawadhalilisha waasisi wa taifa letu si wengine bali Kikwete na genge lake walioendekeza ufisadi, ujangili, ubabaishaji, urongo, usanii na kila aina ya utapeli. Tumieni akili zenu badala ya kuwageuza waasisi hirizi kulinda uchafu wenu. Ama kweli wahenga walisema kuwa PAKA AKIONDOKA PAKA HUJITAWALA!
Si haba Panya aweza kuguguna ngozi ya Simba kwa vile wafu huwa hawasemi wala kujitetea.
 Matembezi ya unazi na ububusa yanapoitwa matembezi ya uzalendo.Ni matembezi ya uzalendo au matembezi ya uzandiki? Mbona hatuoni matembezi kama haya ya kupinga ubabaishaji, ujangili na ufisadi na machafu mengine yaliyotamalaki huku serikali ikiangalia na maafisa wake kuyashiriki?

No comments: