Monday, 28 April 2014

Fanya niwambiavyo na si nifanyavyo mimi

Kwa watu wanaojua jinsi rais Jakaya Kikwete asivyopenda kujisomea, wanashangaa anapopata uchungu na elimu. Japo hii inaweza kuonekana kama kumponda Kikwete, kwa wanaojua alivyoweza kuwakingia kifua mawaziri wake waliotuhumiwa kughushi elimu wanashangaa uchungu wa Kikwete kwa elimu. Kwa waliosahau ni kwamba Kikwete amewakingia kifua  mawaziri Makongoro Mahanga, Mary Nagu na Wiliam Lukuvi na mawaziri wa zamani Emanuel Nchimbi, Deodorous Kamala aliyemteua balozi Ubelgiji. Je mtu wa namna hii anaweza kuwa na uchungu na elimu? Je hii gea ya kutoa vitabu jeshini inalenga kuonyesha nini? Je Kikwete anajiweka karibu na jeshi ili vitisho vyake na Lukuvi vionekane kuwa kweli? Ama kweli alichofanya Kikwete ni sawa na kile cha wahubiri uchwara na wanafiki katika Biblia ambao Yesu aliwakaripia waliokuwa wakiwahubiri watu kusikiliza wawahubiriyo bila kuangalia watendavyo.

3 comments:

Anonymous said...

hii inaweza kuonekana kama kumponda.si inawezekana ndio unamponda hivo au ndio unamsifu.

Anonymous said...

unataka asifiwe kwa sifa ambazo hana ano.

NN Mhango said...

Anon namba moja nadhani jibu umepata toka kwa Anon namba mbili. Kwangu mtu anayekingia kifua walioghushi hawezi kunishawishi bila kuwawajibisha kwanza. Simpondi zaidi ya kusema ukweli. Nilidhani ungekuja na hoja za kuonyesha uongo au udhaifu wa hoja zangu.