Friday, 25 April 2014

Kanada na kufuru ya utajiri.Kanada ni nchi yenye idadi ndogo ya watu lakini tajiri sana. Maisha ya wananchi kawaida nchini Kanada yako juu kuliko hata ya majirani zao kusini yaani Marekani. Kwa mujibu wa Statistics Canada, kwa mwaka wakanada wametumia jumla ya dola bilioni 21.4 kwenye ulabu hadi kufikia mwaka wa fedha ulioishia Machi 31, 2013. Kilichovunja rekodi kwa matumizi kwa wakanada ni sigara ambapo walitumia jumla ya dola  bilioni 31.1 Kamari nayo haikubaki nyuma. Kwani jumla ya dola bilioni 13.74 zilitumika kwenye ka mchezo haka. Mwaka 2006 wakanada walitumia dola bilioni moja kwenye ngono huku mihadarati ikitumia karibu nusu ya kiasi hiki. Hii ndiyo jeuri na kufuru ya utajiri. Nchi yenye watu milioni 34 inaunguza pesa kuliko bara zima la Afrika!

No comments: