Thursday, 17 April 2014

Kama mtoto wa rais alitengeneza bilioni moja baba alitengeza kiasi gani?


Rais wa zamani wa Senegal Profesa Abdulaye Wade amenikumbusha kisa cha maprofesa waliosomea mitihani lakini si kuelimika. Nani alidhani profesa wa sheria angeongoza katika kuvunja sheria tena akiwa rais aliyeapa kuzilinda? Mwana Karim anashikiliwa korokoroni baada ya kufichuka kuwa aliweza kutengeneza au tuseme kuuibia umma fedha kiasi cha Dola 1,400,000,000. Wengi wanajiuliza: Kama mwana ndani ya miaka 12 ya utawala wa baba yake ameweza kuiba kiasi kikubwa hivyo, huyo baba au mama wameiba kiasi gani? Je waramba makalio yao nao wamechota kiasi gani? Maswali ni mengi kuliko majibu. Hii ndiyo faida ya kuchagua upinzani. Vinginevyo, kama upinzani usingeshinda katika Senegal ujambazi kama huu usingefichuka hata kidogo. Je Afrika inao akina Karim wangapi? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: