Monday, 14 April 2014

Hati ya muungano serikali ilivyoishiwa


Kinachoitwa hati ya muungano (pichani) mbona wino kwenye saini ya Mwalimu Nyerere kama wa jana ikilinganishwa na wino kwenye saini ya mzee Abeid Karume? Je hii ni hati halisi au mchakachua.
Inashangaza kuwa na serikali ya wababaishaji na matapeli hata kwa vitu visivyohitaji elimu wala utaalamu sana. Kama hati husika ni original basi wahusika watapaswa watwambie hii tofauti ya wino inasababishwa na nini au wanataka carbon 14 itumike? Japo ni mapema, kuna uwezekano saini ya mwalimu imeghushiwa na kama hii imefanyika basi tunajenga taifa la wahalifu na hatari.

2 comments:

Jaribu said...

Ndio kila siku nasema tunatawaliwa na majuha. Kwanza ilikuwa United Nations, mara itaonekana baada ya siku mbili, na sasa ndiyo hiyo saini ya kughushi. Labda walikuwa wanasubiri wino ukauke.

NN Mhango said...

Jaribu umeniacha hoi. Eti walikuwa wakingoja wino ukauke? Kweli ni majuha tena wa majuha maana kila kitu ni obvious kuwa saini ya mchonga imechongwa.