Tuesday, 29 April 2014

Sauti ya ukombozi iliyozimika Kameruni

Kwa wanaliofuatilia muziki uliowasumbua watawala majambazi wa Afrika watakuwa wanamfahamu nguli Lapiro de Mbanga, mwanamuziki aliyefungwa sana kutokana na vibao vyake vinavyousuta usultani wa kiafrika ambapo ofisi ya rais hugeuka mali ya familia. Kwa wanaojua kifaransa kibao hiki ni ushahidi wa Mbanga alivyopinga utawala wa kijambazi wa Yes Papa au Ndiyo Mzee. Mwaka 2008n aliingia matatani baada ya kufyatua kibao kiitwacho Constitution constipĂ©e” (“Constipated Constitution”)kilichomkosoa imla wa Kameruni Paul Biya. Huyu jamaa unaweza kumlinganisha na Bob Marley ingawa hawakuwa na umaarufu sawa. Hoja zao hazikutofautiana sana kuhusiana na ukombozi hasa wa Fikra. Mungu amlaze mahali pema peponi Lambo Sandjo Pierre Roger (April 7, 1957 – March 16, 2014), aka Lapiro de Mbanga.

No comments: