Friday, 18 April 2014

Mlevi kutangazwa mlevi boraBaada ya kugundua mbinu mpya ya kuongeza ujiko ili kuendelea kuwaibia walevi baada ya kuchemsha, mlevi ameingia na sayansi mpya. Najua wengi wanauliza hii ni sayansi gani? Simple, unaongea na washikaji wako wenye NGO za kusaka ulaji kitapeli wakupe kitu kama tuzo nawe unawapa chochote kitu na mambo yanaishia hapo.
Unapata ujiko wako huku wasiojua ‘chess’ nzima wanaamini sifa unazopewa unazo hata kama huna.
Wajinga ndio waliwao au vipi? Isitoshe si kila ving’aravyo ni dhahabu au goride au gold kwa ndugu zangu wa Malawi na Zimbabwe.
Hivyo, mlevi nimeamua kuchonga na ndugu zangu pale kwa Joji Kichaka wanitafutie NGO ya kunipa ujiko kwa vile nchi ile inaaminika kwa kusaka pesa kwa njia zote halali na haramu.
Bibie Libe Mura-muula aka nshomile upo maeneo ya Washing tone?
Nashukuru sana kwa vile mliwezesha bi mkubwa nami kupata tuzo na nafasi ya kuja huko majuu kushangaa shangaa na kukagua akaunti zetu. Nawashauri muendelee kutafuta wengine wenye kutaka ulaji kwa sharti la kutupa tuzo za hili na lile hiki na kile hata kama ni usanii mtupu.
Baada ya kutumia sayansi hii adhimu ya nyuma ya pazia mlevi nategemea kupewa tuzo ya kuweza kuwa mlevi wa kwanza tena kapuku kuzunguka mabaa yote ulimwenguni nikinywa kama akina Bill Gates bila kumsahau bi mkubwa ambaye huwa anaandamana nami kufanya matanuzi na shopingo aka shopping.
Sina haya ya kuongeza deni la walevi ‘pointlessly.’
Naona yule anatikisa kichwa na kudhania mie ni hamnazo na mpenda sifa kama Dk. Ziro wa kwenye hekaya za Oz.
Yule naye anadhani hizi ni kamba ajue mkono unaenda kinywani ukiachia mbali ujiko usio na utata ninaopata. 
Tuliza majeshi bro au sisie kama si shosti.
Mwenzio ‘soon’ nitapewa tuzo nyingine Bab kubwa ya kutumia sana njuluku za walevi na kufanya wafanye kazi zaidi na kuchangia matanuzi yangu.
Eneo jingine ninalotegemea kuniletea maujiko hata tuzo na maandamano ya walevi na wavuta bangi kunipongeza ni kutokana na umahiri wa kuweza kutoa ahadi nyingi ya kuwapa ofa walevi kuliko kiongozi yeyote wa walevi aliyewahi kutokea.
Japo ahadi hizi hazina uhakika kama ni za kweli au kamba, weye yakuhusu nini haya? Wajinga ndiyo waliwao. Lazima nami niwafaidi au vipi? Kwani kuna ubaya gani kuwala watu ambao wako tayari kuliwa? Kuna tatizo gani kuwala watu wanaojirahisi na kujitia kimbele mbele kama wale mabinti wa shule za msingi aliosema mkuu kuwa wanamimba kutokana na kiherehere chao japo madai kama haya ni kashfa.
Hayo tuwaachie wenye mabinti waamue kama ni kumponda na kumchukia jamaa au kujifanya hamnazo wakampenda badala ya kumponda na kumkaripia asirudie ili liwe somo kwa walevi wengine wa maulaji.
Eneo jingine ambalo lina ujiko wa wazi wazi usio na pingamizi wala mizengwe ni  kutokana na kuandaa utaratibu wa walevi kupata mwongozo mpya wa jinsi ya kulewa na kupambana na ndata.
Hili halijawahi fanywa na kiongozi yeyote wa walevi. Hili ni sawa na kuandika Katiba mpya ya walevi ambapo anayefanya hivyo hupata ujiko na kuheshimika sana kwenye midani ya mibangi na ulevi. Hata hivyo, ‘this move's its risks.’ Ukiamua kuandaa mwongozo mpya kwa walevi uhakikishe huuchakachui wala kujiingiza kwenye malumbano ya mwelekeo gani ufuatwe.
Hapa ukifanya kama alivyofanya mchovu fulani kule Idodomya kwa kukandia mapendekezo ya tume yake, walevi wanakutokea na michupa ili wakutie ngeu.
Uzuri wangu ni kwamba nitatumia njuluku ya walevi kwenda au kutuma makuwadi wa kupokea tuzo yangu. Kwanza,  lazima nitumie ili walevi wachange zaidi.
Lazima kuwepo gharama kwenda kukusanya ujiko wangu toka kwa Wanigeria wangu wanaotaka niwapigie ndogo waje kayani kula bila kutoa jasho kama wale waliokamatwa Tabata wakijifanya kuhubiri dini wakati ni wezi wa kawaida.
Nategemea kupata tuzo nyingine kutokana na kulea vizuri.
Nimefanikiwa kuonyesha kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka na nyoka mtoto ni nyoka na nyoka mzee alikuwa mtoto au vipi? Hivyo, nimewezesha kitegemezi changu kuanza kuukaribia ukuu kwenye kanywaji baada ya kukubaliwa na walevi achukue nafasi yangu ya zamani kwenye bunge la kanywaji. 
Kidume ameonyesha umahiri wa kupiga kanywaji na kupuliza mibangi.
Kuhakikisha hili linafanikiwa, nilitumia raslimali zote za walevi kumpigia kampeni kitegemezi wakati wa harakati za kugombea kiti changu kwenye kijiwe cha walevi.
Kimsingi, tuzo yangu ni tofauti na tuzo nyingine. Kwani kwa kutambuliwa na mataifa ya nje jinsi anavyolewa kistaarabu bila uchoyo ni kielelezo cha ukarimu wangu kuwa nikipiga mma napiga na kila mmoja mwenye ubavu wake hata kufanya hivyo kama kunawaumiza wengine.
Nani anajali iwapo wajinga ndio waliwao? Kwani huwaruhusu walevi kila mtu ajinywee atakavyo bila kujali kama wengine, hasa wadogo, wamepata au wamekosa kanywaji.
Naona yule anakandia kwa kusema eti tuzo yenyewe ni kipande cha kioo.
‘Well and good dude.’ We kipande chako cha kioo kiko wapi?
Wenzio hawaoni unachokiona. Japo kipande cha kioo ni cha hovyo, wenzio wanaona ni tunu na lulu. Hakika wajinga ndio waliwao! 
CHANZO: NIPASHE April 19, 2014.

8 comments:

Anonymous said...

Tunzo kapewa na mafidadi na wezi wenzake
eti anasema wanakukashu Nyerere na karume hawana adabu kwa nyerere na Karume mi miungu si binadam kama mimi yeye na wengine makosa yao lazima yasemwe asante TINDU LISU nakisifu kwa ushujaa
CCM viongozi wengi wanafiki huenda kwenye kaburi la nyerere na karume kuwanga

NN Mhango said...

Anon heri umeliona hilo ingawa watu wetu walio wengi hawalioni hivyo. Tunaendelea kuumizwa na wakoloni na matapeli wa kutengeneza wenyewe. Kikwete hafai kuitwa kiongozi acha kuwa kiongozi bora.

Anonymous said...

Huyu mtu nadhani something wrong down stairs....or both down and upstairs! Haiwezekani mtu akawa anapenda attention kiasi hiki. Hadi kufikia kudanganya wanachi na tuzo za uongozi bora....Na sie watanzania sijui tukoje watu wote wanaamini na kumpongeza. Kwanza kwanini tunzo itoke kwa Balozi ya Naigeria? Hawajui mambo ya itifaki? Aache kutufanya watanzania wajinga kwa kuwa yeye ni mjinga......

Jaribu said...

Halafu alivyong'ang'ania? "Hii tuzo nimeauma niwape wananchi wa Tanzania." Negro please!

Na Nigeria si wana ubalozi Tanzania? Of course wakiarrange dili Tanzania kila mtu atawashtukia, besides utapata wapi trip kama ukifanya utapeli wako Tanzania? Na mimi wanachonikatisha tamaa Waswahili ni kuwa pamoja na taarifa ya habari kusema kuwa tuzo imetolewa na Wanigeria, bado watu wamejikita tu kuwa hawa Wazungu wanataka mali asili yetu, n.k.

Na siyo kwamba wazungu hawawezi kufanya hivyo, tatizo ni kwamba kwa Wazungu ukiwa unapenda sifa za kibuda namna hiyo unaonekana una kasoro fulani, tapeli au una arrested development. Kwa sababu mtu mwenye akili timamu hauweiz kuwa kila siku unapenda kuvikwa kilemba cha ukoka. Huonekani mjanja ila unaonekana na upeo mdogo.

NN Mhango said...

Ukisema hatuna rais bali rahisi wanasema eti unamkosea adabu rais wakati yeye mwenyewe hana hata hiyo chembe ya adabu. Kama anasema hiyo tuzo yake ya kipuuzi amewapa wananchi, mwenzenu simo. Maana nina macho na akili na najua chess nzima. Tuombe Mungu huu mzigo utuondokee uende ukamalizike huko na ukimwi maana it is more than too much. What historic accident! Wakati mwingine huwa nashawishika kusema huyu jamaa ni kiwete upstairs ambaye tunamuita Kikwete bahati mbaya.

Anonymous said...

Kaka Mhango..huyu si mtu wa kuongoza hata MBUZI!! Hana washauri halafu ni mswahili/mshamba/mpenda malumbano na mipasho a.k.a taarabu. Sijawahi ona raisi mwizi kiasi hiki...najua wapo wengi wezi lakini huyu anachukua wazi na watu wanaangalia. Siwezi sema wa kumsamehe ila naamini kuwa malipo ni hapa hapa duaniani...

Anonymous said...

Na kwa nini Membe kakunja ngumi? Hata yeye anafahamu kuwa hamna "tuzo" hapo ni uhuni tu.

NN Mhango said...

Anon hapo juu mmeeleweka. Eti hafai hata kuongoza mbuzi! Hii ya Membe kukunja ngumi sikuwa nimeinyaka.