How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 11 May 2012
Hivi Mwenge bado una maana kwa watanzania wa sasa?
Sisi tunataka kuwasha Mwenge
Tunataka kuwasha Mwenge
Na kuuweka juu ya mlima ooo
Mlima Kilimanjaro.
Kuwasha Mwenge
Kuwasha Mwenge
Na kuuweka Kilimanjaro
Umlike hata nje ya mipaka yetu uletee tumaini
Upendo mahali ambapo pana chuki
Heshima ambapo pamejaa dharau
Matumaini na kadhalika
Haki penye dhuluma
Maadili penye madili
Endelea.
Kwa waliosoma zama zetu huo wimbo ingawa umeongezwa vionjo ulikuwa maarufu hasa wakati ule Tanzania ikijenga jamii huru na ya watu walio sawa. Mwenge wa Uhuru ulihamasisha hayo. Je kwa sasa wakati Tanzani imegubikwa na ufisadi, usanii, kujuana, kulipana fadhili na kuhujumu uchumi bila kuguswa, kweli Mwenge bado una maana yoyote zaidi ya kuwa kejeli kwa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea iliyopinduliwa na Uhujumaa na Kujimegea?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment