Watoto wa rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan na Miraj wakiangua vicheko walipohudhuria sherehe za kuwaapisha mawaziri wapya. Je kiprotokali wameudhuria kama nani? Wapo wanaosema huu ni utawala wa kifalme uliojificha nyuma ya demokrasia. Je hao wananachi wa kawaida walihudhuria kwa msingi upi? Je haya ni matumizi haya mabaya ya madaraka au ni stahiki yao? Blogu hii imeona mjadala mkali kwenye JF kuhusiana na suala la watoto wa Kikwete kuhudhuria uapishwaji wa mawaziri wapya. Je wao kama watu wazima bado wanaweza kuhudhuria kama watoto wadogo wa Kikwete wanaoishi naye ikulu wakati wanaishi na wake zao? Wapo wanaoona kama ni kosa huku wengine wasione kosa. Wapo wanaoonya kuwa na kuuliza swali moja kuu: Je watanzania watarudia kosa kuangalia sura badala ya sifa kwenye uchaguzi? Tutafakari
How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Monday, 7 May 2012
Watoto wa Kikwete na hafla za ikulu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment