Majengo ya kisasa yanayochipuka jijini Luanda Angola.
Hakuna ubishi kuwa nchi zilizokuwa zimeharibiwa na vita kama Angola na Msumbiji kwa muda mrefu sasa ndizo tumaini la uchumi wa Afrika. Hivi karibuni uchumi wa Angola umekadiriwa kuwa mojawapo ya uchumi utakaokua kwa kasi dunia kwa kiwango cha 8%. Hata ujenzi wa majumba kwa sasa kwa mfano kwa mji mkuu wa Luanda uko juu kuliko hata baadhi ya nchi za Ulaya. Kadhalika nchi kama Msumbiji nayo si haba ingawa si kwa kiwango cha Angola. Sudan ya Kusini kama ikitulia nayo yaweza kuwa injini nyingine ya uchumi wa Afrika. Je Afrika inazaliwa toka kwenye majivu wakati nchi ambazo zimekuwa imara kama Tanzania zikielekea kwa majivu kutokana na ufisadi? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.
No comments:
Post a Comment