Taarifa za vyombo vya habari za
hivi karibuni zilipasha kuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja
, katibu mkuu wa zamani wa CCM Yusuf Makamba na mshauri wa zamani wa rais
Kingunge Ngombale Mwiru walimshambulia waziri mkuu Mizengo Pinda hadi kumtaka
ajipime na kuwajibika. Sababu wanazotoa eti kama mawaziri wanne waliwajibishwa
kutokana na ufujaji wa pesa za umma ulioibuliwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa
pesa za serikali (CAG) basin a waziri mkuu awajibike.
Kwani serikali ni iliyofanya
madudu ni ya Pinda au Jakaya Kikwete?
Kwanini hawahoji kubaki kwa
mawaziri wengine waliotuhumiwakama vile George mkuchika na Adam Malima?
Kwanini hawamuhoji Kikwete
kutowawajibisha mawaziri hawa?
Je kati ya Kikwete na Pinda nani
anamhitaji mwenzake?
Wamesahau kuwa Pinda aliokoa
jahazi la Kikwete baada rafiki yake Edward Lowassa kuchafuka? Wanakimbilia
kwenye mashina huku wakiogopa shina je huu si unafiki au wametumwa na mitandao
yao kuanza kupayuka. Waziri mkuu amefanya vizuri kutowajibu maana
angewapandisha chati.
Mbona hawahoji CAG kutosema
ukweli kuhusiana na mahesabu ya jeshi au ofisi ya rais ambayo inajulikana kwa
ufujaji kuliko hata hizo wizara nyingine ambazo mawaziri wake wamewajibishwa?
Kwanini hawahoji ukimya wa
Kikwete kila unapozuka mgogoro hasa ufisadi?
Kwanini hawahoji malipo anayopata
Lowassa ya ustaafu wakati hakustaafu?
Kwanini hawaelezi wazi wazi kosa
la Pinda badala ya kuzungukazunguka kama siyo visa na unafiki na kujikomba kwa
Kikwete? Ukweli ni kwamba hawamsaidii wala haitawasaidia.
No comments:
Post a Comment