Sunday, 27 May 2012

Kumbe Zanzibar tatizo si muungano bali udini?Baada ya polisi wa kupambana na ghasia kutunishiana mikono na kundi la JUMIKI au Jumuia ya Uamsho na  Mihadhara ya Kiislamu kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG) la mtaa wa Kariakoo Zanzibar limechomwa usiku wa kuamkia leo. Je hii ni bahati mbaya au kuna ushirika wa kundi hili linaloanza kutishia amani ya nchi? Tunaambiwa watu wasiojulikana wamechoma kanisa hili. Je kweli waliochoma hawajulikani wakati dalili zote zinaelekea kwa JUMIKI? Kuna haja ya serikali kuwa serious na kundi hili ambalo lina kila alama za kigaidi. Hata Al Shabaab ilianza hivi. Maana bado kuna wendawazimu wanaodhani nchi inaweza kutawaliwa kidini. Hii si karne ya saba na kumi na nne.Je tatizo la Zanzibar ni muungano au udini?

4 comments:

Anonymous said...

Tanzania haina dini .
lakini jumamosi na juma pili ofisi za serikali mashule yote yanafungwa
wasabato jumamosi wa kristo jumaa pili
"LAKINI TANZANIA HAINA DINI"
CHONGO NA KIPOFU BORA CHONGO

tatizo la zanzibari ni muungano ndo uloleta UDINI

Anonymous said...

Kuhusu kuchomwa moto kwa kanisa na gari la Askofu hapa kuna kitu kimejificha.ni mchezo umechezwa ili kuwaharibia JUMIKI waonekana issue kumbe suo Muungano ni Ukristo.madai yao yanajulikana wanataka zanzibar iliyo huru. Haya mapya yanayoibuka ni mbinu za kuwadhoofisha sababu jamaa walianza taratibu sasa wanatisha.na wewe mwenye Blog hii usikurupuke tu kuzungumza usiyoyajua. Inaonekana hata kama shule umeenda lakini haijakusaidia.Pole sana.

NN Mhango said...

Nwashukuruni nyote mliopita hapa na kutoa dukuduku lenu. Ujumbe umefika na karibu tena kila mpatapo fursa. Maana sisi hatuchagui maoni bali kuchapisha kila maoni bila kujali kama tunayenda, kukubalina nayo au la.

Anonymous said...

Muogope kama ukoma anayechanganya dini na siasa ........... vyote ni harakati za kimaisha...... But they always differs tremindously as far as Binadamu is concerned !!!!!!!!
Kutoilinda miiko yote ya ubaguzi,kwa kisingizio cha ukabila,udini,akili nyingi,wehu,kumjua sana mungu wako,etc ni Kutikisa nguvu kuu ya msingi kabisa,ya Umoja wa Taifa la Tanzania iliyojengwa kwa miaka miaka mingi .....Na kuacha mwendawazimu,aendelee na ufujaji wa hazina hiyo,hata kwa dakika moja ni Kosa Kubwa zaidi kwa Msingi huu mkuu kwa Taifa la Tanzania.Kupendana,Kukubali tofauti zetu,na yote yanayofanana na hayo,ndiyo yaliyotukomaza Kimshikamano......