How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 15 May 2012

Tumegeuka taifa la kuchakachua na kughushi




Taarifa kuwa zoezi la kutoa vitambulisho vya utaifa limesitishwa baada ya kugundulika majina mengi ya wanajeshi na polisi kutumika mara mbili, ni pigo kwa usalama na mstakabali wa taifa letu. Kwa mujibu wa vyombo vya habari ni kwamba jumla ya wanajeshi 248 na polisi 700 wanafanya kazi kwa kutumia vyeti vya watu wengine. Hii maana yake ni kwamba walighushi na wapo kazini kinyume cha sheria. Je ni kwanini walipata mshipa wa kufanya hivi? Kwani wao wajinga? Wanajua kuwa kuna viongozi wao wengi walioghushi hasa mawaziri na hawafanywi kitu. Wanajua kuwa serikali wanayoilinda iliingia madarakani kwa uchakachuaji. Wanajua kila kitu kiasi cha kutoogopa chochote.  Je namna hii usalama wa nchi yetu haupo hatarini? Fikiria wanajeshi na polisi wanaghushi na kuambiwa eti wasimamie sheria. Sasa wamegundulika. Unadhani watachukuliwa hatua? Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

No comments: