How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 16 May 2012

Shibuda somo kwa CHADEMA

Mwishoni mwa wiki iliypita Mzee Mustafa Sabodo ameahidi kuzungumza na familia yake ili kuisaidia CHADEMA kujenga jengo jipya la Makao Makuu.

Ingawa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa kikijisifu na kusema kuwa kinaweza kumpokea yeyote atakayehama Chama Cha Mapinduzi (CCM), msimamo huu utakibomoa na kukiangamiza kama hakitabadilika. Hii itakifanya kuwa sawa na kokoro au msafara wa mamba ambao haukosi kenge. Hivi karibuni mbunge wa Maswa John Shibuda (CHADEMA) aliibukia kwenye kikao cha  Halmashauri  Kuu ya CCM akikipigia debe huku akiwaponda wapinzani kikiwemo chama chake. Kimsingi Shibuda ametoa somo kwa CHADEMA kuwa siyo kila asemaye Bwana Bwana atauona ufalme wa Mungu. Wengine ni nyemelezi na mapandikizi kama alivyothibitisha Shibuda ukiachia mbali wengine kama Augustine Mrema, James Mbatia, John Cheyo na wengine wengi. Hivyo CHADEMA, kama itaendekeza tamaa ya kupata wanachama wengi, itaishia kujipaka kinyesi. Na Shibuda si wa kwanza wala wa mwisho. Hata mfanyabiashara wa kihindi mwenye utata Jaffar Sabodo ambaye ameonyesha mapenzi ya ajabu kwa CHADEMA kwa kukimwagia pesa ambayo haulali na uharamu wake ni sawa, anapaswa kuangaliwa kwa jicho la tahadhari.

No comments: