The Chant of Savant

Saturday 12 May 2012

Wazungu wanaogopa uzee hata ukweli


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hilary Clinton alijikuta kwenye hali ngumu baada ya vyombo vya habari kumshambulia kwa kuonekana bila kujipodoa ili kuficha uzee wake. Hivi karibuni akiwa nchini Bangladesh, Clinton aliamua kujitokea bila mikolezo ya mikorogo na vipodozi kama wengine wanavyofanya kuuukimbia uzee wao. Hili lilimsababishia matatizo makubwa kiasi fulani ingawa inavyoonekana hakujali. Kimsingi wenzetu wanapenda sana kuficha hata umri wao ili wasijulikane wazee ingawa uzee hauepukiki sawa na kifo. Wanapendwa kuitwa wasichana na wavulana hata mtu kama ana miaka zaidi ya 70. Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kusema kweli mimi siwaelewi kabisa. Sijui hawajafikiria na fesha kiasi gani wanapoteza. ???

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hiyo ndiyo hasara ya kuishi kwenye dunia ya Alinacha. Ila kwa vile ni weupw, it is Okay.