The Chant of Savant

Sunday 6 May 2012

Tunalaani uteuzi wa wafuatao kwenye baraza la mawaziri

Hon. Soph...Minister ...Image DetailGeorge Mk...
Hakuna kitu kimetuudhi na kutustajabisha kama uteuzi wa mawaziri makapi hata mapanya uliofanywa hivi karibuni rais Jakaya Kikwete. Hii, ima ni kutokana kiburi au kutojua, hatujui. Mawaziri kama Sofia Simba, Steven Wassira, Mathias Chikawe, William Lukuvi, Celina Kombani, Hawa Ghasia, Jumanne Maghembe,Emanuel Nchimvi George Mkuchika, Matayo Matayo Mary Nagu na Hussein Mwinyi hawakupaswa kurejea kutokana na madudu yao kuanzia kughushi vyeti vya taaluma hadi kubebwa tu kwa vile ima wana uhusiano mzuri na rais au mkewe.
Manaibu mawaziri Adam Malima, Lazaro Nyalandu na  Makongoro Mahanga hawakupaswa kurejea kama siyo kulindana. Wamerejeshwa kwa lipi wakati wamejaa uvundo nyuma yao? Hivyo, kwa ufupi, tunapinga uteuzi huu wa kishikaji kwa herufi kubwa. Shame on you all the appointees and the one making appointment. 

No comments: