How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 4 May 2012
Baraza kuu kuu la mawaziri na recycling usanii na dhihaka
Kwa waliosikia au kusoma orodha ya baraza la mawaziri tuliloahidiwa kuwa lingesukwa upya na kuja na mapya watakuwa wamepigwa na butwaa juu ya kiburi na ugumu wa rais Jakaya Kikwete kujifunza. Kimsingi alichofanya Kikwete ni kile watoto wa mjini huita changa la macho. Kwa blogu hii kilichofanyika ni usanii na dhihaka kwa watanzania. Tuna sababu za kusema hivyo;
Mosi, zimerudishwa sura zile zile hata ambazo zina madhambi ya wazi wazi na ya muda mrefu.
Kwa mfano unategemea jipya gani kutoka kwa watu kama Stephen Wassira, Jumanne Maghembe, Matayo Matayo, Mathias Chikawe, Celina Kombani, Sofia Simba, Adam Malima na wengine wengi.
Pili hatukuamini kama rais angewarejesha watuhumiwa wa kughushi ambao wanajulikana kuwa ni Makongoro Mahanga, Mary Nagu na Wiliam Lukuvi.
Tatu, rais amelazimika na kupoteza imani na muda wetu bure. Tulitegemea mapya lakini ameturejeshea mvinyo ule ule kwenye chupa ile ile. Hivi rais wetu atajifunza lini wakati muda ukizidi kuyoyoma? Je wabunge waliotunisha misuli na kuondoa baadhi ya mawaziri wataridhika na dhihaka hii? Kwanini rais hakufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri badala ya kutupotezea muda na kutuweka kwenye sintofahamu kwa muda mrefu. Hakika kilichofanyika licha ya kuwa dhihaka na usanii, ni taarifa kuwa Tanzania itazidi kuendelea kuelekea kuzimu.
Tumewahi kusema kuwa serikali ya Kikwete ni ya ubia na kuna watu wenye shares nyingi. Nao ni hao ambao hawagusiki bali huwa recycled kila mara.
Mfano mdogo ni kwamba kwa mazabe na madudu aliyotenda mtu kama Adam Malima, kama siyo kulindana kwa misingi yoyote iwayo hakupaswa kurejeshwa au tuseme kuwa recycled.
Hakika hili si baraza jipya la mawaziri bali baraza kuukuu na la kishikaji na Jakaya Kikwete. Kweli Tanzania tunayo safari ndefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment