The Chant of Savant

Tuesday 15 May 2012

Unaweza kuamini yeyote isipokuwa malaya na mwanasiasa

Francois Hollande and Angela Merkel (15/05/12)
Kwa wale waliofuatilia uchaguzi wa hivi karibuni nchini Ufaransa ambapo rais mpya Francois Hollande alimbwaga rais wa zamani Nicolas Sarkozy, watakumbuka msoshalisti Hollande alivyoshinda kiti cha urais kwa kuponda sera za kiuchumi za Sarkozy.
Kosa kubwa alilotenda Sarkozy ilikuwa ni kukubaliana na sera za kubana matumizi zinazopendekezwa na chansela wa Ujerumani Angela Merkel. Ushirikiano wa Merkel na Sarkozy ulibatizwa jina la Merkozy. Ajabu ya maajabu ni kwamba Hollande baada ya kuingia madarakani amemuahidi Merkel kuhakikisha anashirikiana naye kutatua matatizo ya kiuchumi ya Ulaya. Kwa maana nyingine ni kwamba kifo cha Merkozy kimezaa Hollamer au tuseme Merholla! Kwa wenye kumbukumbu wanashangaa Hollande ameruka nini na kukanyaga nini? Ama kweli unaweza kumwamini yeyote isipokuwa malaya na mwanasiasa. Leo anasema hili kesho anasema lile na ukimuuliza kuhusu yote anaruka na kuja na yale? Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

No comments: