The Chant of Savant

Friday 11 May 2012

Kenya yafuta vyeo vya mkuu wa mkoa na wilaya



Hakuna ubishi kuwa wakuu wa mikoa na wilaya nchini wana madaraka makubwa na marupurupu makubwa yasiyo na faida kwa mlipa kodi. Ukichunguza umuhimu na kazi zao unapata hitimisho kuwa ni marais wadogo walioteuliwa na rais mkubwa ili kuendeleza ukandamizaji na unyonyaji kwenye maeneo yao. Kenya ililiona hili na kuondoa vyeo hivi ambavyo kimsingi kwa nchi kama yetu zinazoving'ang'ania ni kukaribisha umaskini wa kujitakia. Je umefika wakati wa Tanzania kuondoa vyeo hivi haramu vinavyotumiwa kama uchochoro wa rais kulipa fadhila kwa jamaa na marafiki zake na kuliingizia taifa hasara? Pia wakuu wa mikoa na wilaya wanasifika kwa kukandamiza upinzani na kunyanyasa wananchi. Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

No comments: