The Chant of Savant

Friday 18 May 2012

Kiongozi wa nchi anapochorwa uchi na mwananchi

Stephen Harper Nude
Mchoraji wa kike Magreth Suthrtland hivi karibuni alimchora waziri mkuu wa Kanada, Stephen Harper akiwa uchi na kutundika picha yake kwenye maktaba ya umma. Kwa wanaokumbuka kilichowatokea watu walioonyesha picha za kiongozi fulani akiwa uchi watashangaa uhuru huu wa kujieleza. Tunajiuliza. Hili lingefanyika Afrika mchoraji angekuwa kwenye hali gani iwapo hata ukimwambia ukweli kwa mfano kiongozi fisadi mkewe au familia yake unaonekana mchochezi? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA. Huko Afrika Kusini picha kama hii imesababisha wanasheria wa rais kutishia kumshitaki mchoraji aliyechora picha ya rais Jacob Zuma akionekana kama Lenin huku  nonihino yake ikining'inia. SOMA HAPA.
Hivi Zuma huwa anajali wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka? Hebu angalia alivyovaa ngozi ya chui. Je rais kama huyu anaweza kuwanusuru wanyama hawa au kuwamaliza?

No comments: