Kuteuliwa kwa mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia kuwa mbunge ni muendelezo wa siasa za kulipana fadhila hasa baada ya wahusika kuwa makapi. Mbatia licha ya kushindwa kwenye uchaguzi, anadhihirisha uvumi uliowahi kuwapo kuwa ni pandikizi la CCM kwenye upinzani. Ingawa si shurti kwa rais kujieleza anapomteua mtu wake, uteuzi wa Mbatia unaacha maswali mengi kuliko majibu. Je NCCR-Mageuzi ni CUF au hata TLP nyingine na Mbatia ni Shariff Hamad au Augustine Mrema mwingine ambaye yuko radhi akitoa chama kafala kwa sababu ya ulaji binafsi? Je hapa rais hajaanza kuuathiri upinzani?
No comments:
Post a Comment