Friday 4 May 2012

Baraza la mawaziri na watoto wa vigogo

Image Detail
Hussein M...
    Mheshimiw...

Katibu mkuu wa zamani wa CCM Yusuf Makamba aliwahi kujivuna kuwa amezaa watoto wenye bongo na hivyo lazima mwanae awe waziri. Kikwete alipovunja baraza la mawaziri kutokana na kipenzi rafiki na mshirika wake Edward Lowassa kusombwa na kashfa ya Richmond, alimuacha nje January. Hii ilifanya watu tumzodoe Makamba kuwa yako wapi tusijue kuwa waarabu wa Pemba hujuana kwa viremba! Sasa January pamoja na uteke wake ni waziri. Anazidi kutunisha namba ya watoto wa wakubwa walioridhi ukubwa wa wazazi wao. Leo tuna Emanuel Nchimbi mtoto wa kigogo wa zamani wa CCM, January Makamba kadhalika, Adam Malima mtoto wa swahiba mkubwa wa rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye mwanae ni waziri wa Afya na Hamis Kageshiki mkwe wa Mwinyi. Kimsingi, Makamba hakutabiri wala kubabaisha bali alijua walivyo na hisa kwenye serikali hii ya kishikaji ya kujuana na kulindana ukiachia mbali kulipana fadhili kwa mgongo wa jasho la mlipa kodi maskini. Ubaya ni kwamba wale wasio na hisa walipopewa madaraka wakajisahau kuwa hawakuwa na hisa.
Hii ndiyo siri ya kubakizwa kwa watu kama Adam Malima ambaye alishirikiana na William Ngeleja kuhujumu uchumi. Kadhalika Dk. Hussein Mwinyi ambaye mabomu yaliua watu chini ya uangalizi wake na akashinikizwa ajiuzulu akagoma kwa kujua shea za baba yake kwenye serikali. Kadhalika Emanuel Nchimbi anayekabiliwa na shutuma za kughushi vyeti vya kitaaluma. Hawa ni watoto wa wenye hisa hawaguswi wala hawastuki hata wakikosea vipi.

1 comment:

malkiory said...

Dada yake Makamba Jr. ni bosi VODA, mtoto wa Waziri mkuu yupo Utumishi. Raisi wetu ni sikio la kufa halina dawa.