How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 21 May 2012

Kweli Sitta na wenzake wana sura mbili



Vyombo vya habari vimenukuu waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akiwanyoshea wenzake kidole huku akisahau kuwa vingine vinne vilikuwa vimemwelea yeye. Amesahau kuwa historia ya usura-mbili wake ni ya jana na bado ni mbichi kwenye kumbukumbu za Watanzania. Amesahau kuwa Watanzania wanamjua alivyohongwa madaraka yeye pamoja na Dr Harrison Mwakyembe wakawasaliti na kuwauza kwenye kashfa ya Richmond! Ingawa Sitta hakulenga kujenga maana hii, ukweli ni kwamba Sitta na wenzake wana sura nyingi tena si mbili tu. Leo wanakuwa wapiganaji dhidi ya ufisadi. Kesho wanageuka washirika wa uongozi wa mafisadi! Njaa na tamaa nyingine omba usiwe navyo. Maana utavua nguo bure.

Someni mwenyewe nukuu ya Sitta
“Msishangae, tuna viongozi wenye sura mbili, wapo wanaofikiri kwa kutumia matumbo yao jinsi ambavyo wataneemeka na kujinufaisha wenyewe, hawa ni wale wabinafsi lakini wapo viongozi ambao wanatumia ubongo katika kufikiri jinsi ambavyo watatumia uwezo wao wote katika kuwatumikia wananchi, mimi ni miongoni mwa hawa,” 


Wenzake wanatumia matumbo. Je yeye anatumia meno au masaburi?

3 comments:

Jaribu said...

Nyani haoni samahani, kundule.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

You are right Jaribu but one day nyani will truly see his or her butt. Sitta will be one of them so to speak

Anonymous said...

Aso hili ana lile ajichunge