How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 21 May 2012

Kweli Tanzania taifa la matapeli na waganga njaa!

Watu wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila mwenye umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma mwenye umri wa miaka 20 (mwanaume) ambao walitambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha,walikamatwa jana majira ya saa 12 asubuhi katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.


Ingawa ni mapema kusema, ukweli ni kwamba hiki kinachoitwa kukamata wachawi ni utapeli wa wenye kijikanisa husika ili kionekane kina nguvu za ajabu. Kesho utawasikia matapeli walioko nyuma ya kijikanisa hicho wakihubiri kutenda miujiza na kuwaibia watu maskini na wajinga. Kwanini viongozi wetu wa juu wanafumbia macho jinai hii ambayo sasa inaanza kuzoeleka? Hakuna kitu kama kuruka na ungo wala kukamata wachawi bali utapeli wa kuweka watu wajinga kwenye mazingira ya kuonyesha kuwa walikuwa wachawi wakakamatwa kwa nguvu za mchungaji au nabii wakati ni utapeli. Hawa ndio wanaoua mazeruzeru usiku na mchana wakahubiri kukamata wachawi wakati wachawi wakubwa ni wao. Njaa na ujinga vikichanganyika ni balaa. Ni bahati mbaya kuwa taifa letu limegeuka la utapeli, udaku na uganga njaa. Huu ni uchakachuaji wa kiakili so to speak.

4 comments:

Jaribu said...

Ukiwaweka watu kwenye umbumbumbu inakua rahisi kuwatawala.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ila hii ni hatari my friend. Maana njaa inaonekana kuwa kwenye vichwa vya watu wetu kuanzia wadogo hata wanaoitwa wakubwa lakini hovyo.

Anonymous said...

ndugu yangu mpayukaji, kwa nini unakimbilia ku-conclude kuwa huo ni utapeli bila kufanya utafiti wa kutosha? Sikutegema kwa mtu kwa wewe kurukia conclusion bila utafiti. Hao watu wamejieleza wenyewe kuwa ni wachawi, kwa nini wewe uwasemee kuwa sio wachawi, prove it please. If you don't basi na wewe ni tapeli na mwongo, full stop.

Anonymous said...

Si wachawi ni ghilba na mbinu za utapeli zinatumika, unakumbuka Dar wakati fulani dada mmoja alijifanya nchawi halafu wakamrusha dau lake naye akapasua jibu?! Pia unakumbuka baba mmoja toka mbeya alivyofia Dar kwa huo utapeli kwa ujira wa sh. 200,000/=. Kusoma hujui hata picha huoni?